Bifu la Kanye West na Big Sean hali si shwari, Ni muda mfupi tu, baada ya Kanye kuweka wazi kuwa kumsaini kwake Big Sean kwenye Label yake Good Music ni kitu kibaya zaidi alichowahi kufanya kwenye maisha yake.

Kauli hiyo hatimaye imemfikia rapa Big Sean muda mfupi baada ya mahojiano aliyoyafanya ‘YE’ na kipindi cha Drink Champs cha Revolttv, na ameamua kumjibu kwa kuandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa mtandao wa twitter akiambatanisha na picha zenye kumuonye akiwa kwenye mazungumzo na Kanye na kusema kwamba alipata nafasi ya kuonana na muda mfupi baada ya mahojiano hayo lakini Kanye hakumuambia chochote kati ya aliyoyazungumza kwenye mahojiano hayo.

Big Sean ameonyesha kushangazwa na kitendo cha ‘YE’ kumuongelea vibaya, kiasi cha kuandika ujumbe mwingine unaosema kuwa anasubiri kwa hamu kupata nafasi ya kufanya mahojiano na Drink Champs ili naye aweke wazi yenye kuhusu upande wake.

Ndiaye akaribia kutua Simba SC
Kanye west ajutia kumsaini Big Sean 'Good Music'