Mshambuliaji Sadio Mane na Joao Cancelo hawatakuwa na muda mrefu katika kikosi cha FC Bayern Munich na hawatarajiwi kuendelea kuwepo zaidi ya kipindi cha majira ya joto ya sasa.

Bayern wana nafasi ya kumnunua Cancelo, ambaye yupo kwa mkopo klabuni hapo kutoka Manchester City, lakini hawana mpango wa kulipa kiasi cha Pauni milioni 60 (sawa na Sh bilioni 176) kwa ajili ya kumsajili beki huyo Mreno.

Kwa upande wa Mane naye atatolewa katika kipindi hiki cha majira ya joto baada ya kuichezea FC Bayern Munich msimu mmoja, ambao amefunga mabao 12 tu.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Senegal, hajaweza kupata nafasi ya kudumu katika kikosi cha kwanza chini ya kocha mpya wa timu hiyo, Thomas Tuchel na inaaminika kuwa kuna nafasi kubwa mchezaji huyo akarudi katika Ligi Kuu ya England.

Mane ameanza katika mechi sita tu katika kikosi cha kwanza cha FC Bayern Munich tangu aliporejea kutoka katika maumivu Februari, akifunga mara moja tu na mwezi Aprili alifungiwa mchezo mmoja baada ya kukwaruzana na mchezaji mwenzake, Leroy Sane.

5,000 yampa Tsh 20,000,000 kwa kucheza Kasino ya Meridianbet
Pamba FC: Hatutarudia makosa Play Off