Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, amewataka mawaziri wapya walioapishwa kujiandaa kuchapa kazi kwa nguvu zote kwani wakati uliopo sio wa kuzembea.
Ameyasema hayo jana alipokuwa akiwapongeza Mawaziri hao ambao awali wengine walikuwa wabunge wa kawaida na sasa wana kofia za uwaziri, na kwamba wakienda bungeni ni kuchapa kazi tu.
“Mheshimiwa Rais ni matumaini ya watanzania kwamba timu hii ambayo inaimarisha Baraza la Mawaziri na kama tulivyoambiwa hapa wanaanza kazi leo leo kwa kikao cha Baraza la Mawaziri, tunawatakia kila la heri, tunawakiribisheni bungeni, niwaambie neno moja tu mbele yako Mheshimiwa Rais wajiandae, hawa walioapishwa na hawa wengine waliokuwepo, hii miaka miwili ya mwanzo tulikuwa tunachukulia wanajifunza, sasa hivi tukienda Dodoma ni kazi tu,”amesema Ndugai
-
Video: Shirika la posta laipiga jeki taasisi ya moyo (JKCI)
-
Video: Mfumuko wa bei wazidi kupanda
-
Kitila Mkumbo ang’atuka ACT-Wazalendo
Hata hivyo, Rais Magufuli jana aliapisha Baraza la Mawaziri baada ya kulifanyia mabadiliko Oktoba 7, na kuwataka waanze kazi mara moja, huku wakikabidhiana nyaraka za ofisi tayari kwa utekelezaj