Naibu waziri wa afya, Dkt. Faustine Ndugulile amekanusha uvumi wa taarifa kuwa anaumwa, mapema leo Mei 11 na kutoa pole kwa wote waliaothirika na taarifa hiyo.
Kupitia ukurasa wake rasmi wa Twitter amewataka wananchi kupuuza taarifa za ugonjwa juu yake na kuthibitisha kuwa ni mzima na anaendelea na majukumu yake.
“tupuuze taarifa za uzushi zinazosambazwa kuhusu afya yangu. niko mzima kabisa na ninaendelea na majukumu yangu, pole nyingi kwa walioguswa na taarifa za uzushi” ameandika Ndugulile.
Hayo yamejiri baada ya taarifa kuenea kwenye mitandao ya kijamii kuwa naibu waziri huyo anaumwa na amelazwa katika hospitali ya taifa Muhimbili.