Mkuu wa wilaya ya Songea, Pololet Mgema amewatembelea wananchi wa kijiji cha Lugagara mkoani Ruvuma walioshikwa na hofu na taharuki baada ya eneo la ardhi ya hekari tano kutitia mita tano kwenda chini.

Kwa mujibu wa ITV Mkuu wa wilaya hiyo ametoa wito kwa wananchi kuwa makini katika eneo hilo pindi wananpofanya shughuli zao na watafanya uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo kujua limetokanana na nini.

Naye mwenyekiti wa Kijiji cha Lugagara, Daniel Mwinuka amemshukuru mkuu wa wilaya hiyo kwa kuwatembelea na kuwatoa hofu na kwamba watachukua tahadhari kwenye shughuli zao.

Hata hivyo wananchi wamesema hofu yao inakuja kutokana na maeneo hayo kuwa ya kilimo na makazi na hivyo ikiwa eneo lingine lenye watu na makazi likatitia yanaweza kutokea maafa.

Julio aiponda ligi kuu, ashusha kiwango cha Okwi
Corona Uingereza: Wafanyakazi waruhusiwa kwenda ofisini