Mwanasheria wa Kiungo kutoka Visiwani Zanzibar Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’ ameendelea kusisitiza kuwa, Mteja wake hana sababu ya kurudi Young Africans kwa sababu hana Mahaba na Klabu hiyo.
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’ ilitoa taarifa ya kumtambua ‘Fei Toto’ kama Mchezaji wa halali wa Young Africans, baada ya kusikiliza kesi iliyoanza siku ya Ijumaa (Januari 06) hadi Jumamosi (Januari 07).
Wakili wa kiungo huyo, Nduruma Majembe amesema: “Mteja wangu (Fei Toto) hana tena mapenzi ya kurudi na kuendelea kuitumikia klabu yake ya Young Africans.”
“Kwani katika kikao cha kamati aliweka dhahiri kwamba hakuna uwezekano wa yeye kurudi tena kuichezea Young Africans. Labda atafutiwe mwanasaikolojia atakayebadilisha mawazo yake.”
“Nikiri kupokea kwa taharuki na masikitiko makubwa maamuzi ya kamati dhidi ya ‘Fei Toto’ kumrejesha Young Africans, na leo tutajua sababu ambazo kamati zimefanya Kamati ya Sheria na Hadi za Wachezaji kumbakisha Young Africans, lakini pia tunaweza kuomba Review ya hukumu au kwenda moja kwa Moja CAS kupinga maamuzi hayo,” amesema Majembe.