Mmiliki wa Klabu Bingwa nchini Ufaransa Paris Saint-Germain Nasser Al-Khelaifi anatajwa kuwa kwenye mpango wa kuwekeza katika soka la nchini England.

Al-Khelaifi ambaye ni Mfanyabiashara kutoka Qatar, amekua na mafanikio makubwa katika uendeshaji wa Biashara ya Soka kupitia PSG, ambayo ipo chini ya Kampuni yake ya Qatar Sports Investments ‘QSI’.

Taarifa zilizochapishwa katika Tovuti ya Sky Sports zimeeleza kuwa, Tajiri huyo juma lililopita alikutana na Mwenyekiti wa Bodi ya Klabu ya Tottenham Hotspur Daniel Levy, katika moja ya Hoteli yenye hadhi ya Nyota tano jijini London.

Hata hivyo licha ya Sky Sports kuwa na uthibitisho wa kikao hicho, Uongozi wa Spurs umekataa kata kata kuhusika kwenye kikao hicho.

Sababu ambayo Spurs inaitumia kutohusika kwenye Mkutano huo na kuhisi huenda wawili hao walikutana katika makutano binafsi, uliohusu umoja ya Klabu za Barani Ulaya, ambapo Al-Khelaifi ni Rais wa Umoja huo, huku Levy akitambulika kama mjumbe.

Kampuni ya QSI inamiliki sehemu ya hisa za Klabu ya Braga ya nchini Ureno, na imekua ikiendeleza mkakati wa kutaka kumiki sehemu ya hisa za klabu nyingine Barani Ulaya, ambazo zina ushaiwshi mkubwa.

Zaidi wa Klabu 300 Duniani zinatajwa kuwa kuwa kwenye umiliki wa Kampuni QSI, huku Klabu za PSG na FC Braga zikithibitika kuwa kinara kwenye umiliki huo.

Kutajwa kwa klabu ya Spurs kuwa kwenye mpango wa kutaka kumilikiwa na Kampuni ya QSI, ni muendelezo wa uwekezaji ndani ya Klabu za England, ambapo kwa sasa Klabu za Manchester United na Liverpool zipo kwenye mchakato wa kuuzwa.

Watanzania watakiwa kuadhimisha miaka 59 Mapinduzi Zanzibara kwa kupanda miti
Nduruma Majembe: Tutakwenda CAS kusaka haki