Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya mitihani ya Kitaifa ya upimaji wa maarifa Darasa la Nne, Kidato cha Pili na Mtihani wa Taifa wa Kidato cha nne kwa mwaka 2020.
Matokeo hayo yametangazwa leo Ijumaa Januari 15, 2021 Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt. Charles Msonde ambaye ameeleza kuwa katika matokeo hayo wavulana wameongoza katika orodha ya wanafunzi 10 bora ambapo ambayo wapo wavulana saba na wasichana watatu.
Shule ya sekondari Cannosa ndiyo iliyong’ara zaidi kwa kuingiza wanafunzi watatu kwenye 10 bora.
Kulingana na orodha hiyo, Paul Luziga wa Panda Hill ameshika nafasi ya kwanza akifuatiwa na msichana Justina Gerald wa Canossa.
Mwanafunzi wa tatu ni Timothy Segu wa (Mzumbe), Isaya Rukamya(Feza Boys), Ashraf Ally (Ilboru), Samson Mwakabage (Jude), Derick Mushi (Ilboru).
Wengine walioingia kumi bora ni Layla Atokwete (Canossa), Innocent Joseph (Mzumbe) na nafasi ya 10 ikishikwa na Lunargrace Celestine wa Canossa.
Bonyeza hapa kutazama matokeo ya kidato cha nne 2020
Bofya hapa kutazama matokeo ya kidato cha nne 2020