Mshambuliaji kutoka nchini Nigeria a Odion Ighalo, anafikiria kuhamia katika ligi ya Marekani ya MLS, baada ya kukamilika kwa mkataba wake wa mkopo akiitumikia Manchester United.

Ighalo mwenye umri wa miaka 31, alijiunga na Manchester United akitokea klabu ya China ya Shanghai, Januari 2020.

  • Klabu ya Tottenham Hotspurs huenda ikashindwa kumuongezea mkataba wa mkopo mshambuliaji kutoka nchini Wales Gareth Bale.

Spurs walimsajili kwa mkopo mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 31, wakati wa usajili wa majira ya kiangazi akitokea kwa mabingwa wa soka nchini Hispania Real Madrid.

  • Beki wa Brighton Tariq Lamptey mwenye umri wa miaka 21, anakaribia kusaini mkataba wa muda mrefu na klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya England.

Lamptey anatajwa kuwa kwenye mpango wa kusaini mkataba wa muda mrefu kwenye klabu yake, kufuatia klabu kadhaa kuanza kumnyatia.

Mabingwa wa soka Barani Ulaya FC Bayern Munich ni miongoni mwa klabu ambazo zinahusishwa na uhamisho wa beki huyo kutoka nchini England.

  • Mshambuliaji na nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil Neymar da Silava Santos Junior, ameanza mazungumzo ya kusaini mkataba mpya na mabingwa wa soka nchini Ufaransa Paris-St Germain.
  • Klabu za Tottenham na Chelsea zote za jijini London, zina hamu ya kumsajili beki wa kati kutoka Korea Kusini mwenye umri wa miaka 24 Kim Min-jae, ambaye anachezea klabu ya china ya Beijing Guoan.
  • West Ham inafikiria kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Reims na Senegal Boulaye Dia, huku thamani ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 iktajwa kufikia Pauni milioni 15.
  • Klabu ya Aston Villa imedhamiria kumsajili kiungo wa kati wa Bournemouth na Wales David Brooks mwenye umri wa miaka 23, katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili.
  • Klabu ya RB Leipzig haina mpango wa kumuuza beki wa kati wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 22 Dayot Upamecano licha ya kwamba anaweza kuondoka katika majira ya kiangazi kwa dau la Panuni Milioni 37.4.

Klabu za England Liverpool, Chelsea, Manchester United na FC Bayern Munich ya Ujerumani zinatajwa kumuwania beki huyo.

  • Beki wa kulia wa Aston Villa na Ufaransa Frederic Guilbert mwenye umri wa miaka  26, amekataa kujiunga na klabu ya Uturuki ya Istanbul Basaksehir.
  • Klabu ya Arsenal inatajwa kuwa miongoni mwa klabu zinazomuwania winga wa klabu ya Shakhtar Donetsk na Israel Manor Solomon.

Arsenal inajipanga kumsajii winga huyo mwenye umri wa miaka 21, wakati wa usajili wa majira ya kiangazi.

Messi akwaa kisiki Hispania
NECTA yatangaza matokeo ya kidato cha nne 2020

Comments

comments