Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu Prof. Jamal Katundu amesema kanuni mpya ya kikokotoo inaongeza inaongeza kiwango cha mkupuo kutoka asilimia 25 iliyokataliwa mwaka 2018 hadi asilimia 33 kwa zaidi ya wananchama mil 1.3 sawa na asilimia 81 ya wananchama wote wa mifuko amabo ni mil. 1.69.

Profesa Katundu amesema makubaliano ya kikokotoo limbikizi kitakuwa 1/580 kama ilivyokuwa kwa mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na mifuko ya PPF, GEPF na baadhi ya wanachama wa iliyokuwa PSPF na LAPF.

Hatua hiyo imekuja baada ya makubaliano kati ya Serikali, Chama cha Waajiri Nchini (ATE) na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta) bada ya kusitishwa kwa kanuni zilizotengenezwa Desemba 28, 2018,

Amesema mshahara wa kukokotolea mafao ya pensheni utakuwa wastani wa mishahara bora ya miaka mitatu ndani ya miaka 10 kabla ya kustaafu.

Aidha amesema kuwa umri wa kustaafu utaendelea kuwa miaka 60 ambapo ameeleza kuwa kikotoo hicho kitaanza kutumika Julai Mosi mwaka huu.

Majaliwa aigeukia Ardhi, ataka uhakika wa fidia
Moto hospitalini waua vichanga 11