Fashion Association of Tanzania (FAT), imezindua nembo ya umoja wa wanamitindo Tanzania na kuwataka wafanayakazi katika sekta hiyo kujiunga na chama hicho kwa lengo la kukuza sanaa ya mitindo Tanzania.

Mkurugenzi wa Baraza la Sanaa Tanzania, Godfrey Mungereza amezindua nembo hiyo akiongozwa na Mwanzilishi wa chama cha mitindo Tanzania, Mustafa Hassanali.

Mustafa amedadafua kiundani zaidi kuhusiana na madhumuni ya kuanzisha umoja huo wa wanamitindo Tanzania.

Ameeleza kuwa Fashion Associaton of Tanzania, kimeanzishwa kuwa chama chenye nguvu na taaluma yenye uwezo wa kukuza na kuimarisha sekta ya mitindo nchini, kama wabunifu wanaunga mkono juhudi za Rais Magufuli katika kuifanya Tanzania kuwa katika uchumi wa Viwanda wa kati ifikapo 2025 na kuongoza katika bidhaa za nguo na vitambaa Tanzania.

Mmoja ya waanzilishi wa chama hicho, Asia Idarous amesema kuwa chama hiko hakijaundwa kwa ajili ya wabunifu tu bali kwa watu wote katika sekta ya mitindo kwani inajumuisha majukwaa mbalimbali ya mitindo, taasisi za mitindo, wanamitindo wa kuonesha mavazi, wapiga picha wa mitindo, makampuni ya nguo, wazalishaji na wauzaji wote wanaojihusisha katika mitindo na urembo.

Amesisitiza kwamba nchi nyingi zenye maendeleo makubwa katika sekta ya mitindo ni zile zilizounda chama ambacho kinasimamia maslahi yao.

Hivyo amewaalika wanamitindo mbalimbali kujiunga katika chama hicho ili kupata muongozo utaowasaidia kutimiza malengo yao.

 

Mwijage: Ni kweli tunadaiwa lakini hatulipi
Mchakato wa kupata cheti kufanyika ndani ya siku 30