Mtu mmoja afariki na wengine 27 hawajulikani walipo kutokana na mlipuko wa vulkano, huku watu 23 wakiokolewa na polisi wametahadharisha kuongezeka kwa vifo katika tukio hilo lililotokea muda mfupi baada ya watalii kuonekana karibu na mlima huo.
Waziri mkuu wa nchi hiyo, Jacida Adern amesema oparesheni za kuwatafuta manusura zimeanza lakini moshi mkali katika eneo hilo unazuia juhudi za uokoaji.
Mlima ulio lipuka upo katika Kisiwa cha White Island, ambacho pia kinafahamika kama Whakaari, ni moja ya maeneo yaliyo na milima mingi ya volkano. huwavutia watalii ambao huzuru mara kwa mara nyakati za mchana kutokana na kuwepo kwa ndege zinazoendesha shughuli za kitalii.
Desemba 3, mwakahuu wanajiolojia walitahadharisha kuwa mlima huo huenda ukalipuka kupita kawaida yake, japo waliongeza kuwa kiwango hicho cha mlipuko hakiwezi kuhatarisha maisha ya watalii.
Kisiwa cha White Island kimeshuhudia milipuko kadhaa ya volkano katika miaka iliyopita ya hivi karibuni ikiwa na mwaka 2016, lakini hakuna mtu aliyejeruhiwa.
Polisi inaonya watu wanaoishi karibu na na maeno ya hayo kuwa ”waangalifu dhidi ya majivu ya moto na kuwaomba ikiwezekana wasiondoke majumbani mwao”