Wawakilishi wa Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Brazil Neymar wamefanya mazungumzo juu ya uwezekano wa mchezaji wao kuhamia Saudi Arabia, kwa mujibu wa 90min, huku uwezekano wa kurejea Barcelona ukikataliwa na kocha Xavi.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 amebakiza miaka miwili katika mkataba wake na Paris Saint-Germain, huku Uongozi wa PSG ukiwa na chaguo la kumuongeza mkataba wa miezi 12 zaidi.
Lakini Mbrazil huyo mwenye amekuwa akilengwa na baadhi ya mashabiki wa PSG ambao wanachukizwa na uchezaji wake uwanjani na hivi karibuni kulikuwa na maandamano nje ya nyumba yake wakimtaka aondoke katika klabu hiyo msimu huu wa joto.
90min ilifichua mwanzoni mwa Mei kwamba wamiliki wa Newcastle walikuwa wakitafuta uwezekano wa kumchukua Neymar kwenda.
Hata hivyo, vyanzo vimethibitisha kwa 90min kwamba mazungumzo yame fanywa na wawakilishi wa Neymar na wajumbe wanaowakilisha Ligi ya Saudi Pro, ambao wana nia ya kumfanya atue huko Mashariki ya Kati.
Mshambuliaji Karim Benzema alijiunga na Al Ittihad akitokea Real Madrid kwa mkataba wa miaka mitatu Jumanne, huku N’Golo Kante na wachezaji wengine wakipewa fedha nyingi kufuata nyayo za Cristiano Ronaldo aliyejiunga na Al Nassr mwisho wa 2022 ili kuipandisha Saudi Arabia ka- tika umaarufu wa soka.
90min inaelewa kuwa Neymar amepewa ofa ya kwenda Barcelona ambao walikosa kumsajili tena Lionel Messi baada ya kuchagua kujiunga na Inter Miami lakini kocha Xavi alikataa nia ya kumsajili tena, akikimbia kituo cha Twitch kuhusu uvumi huo: “Nimeshangaa… hayuko ka- tika mpango wetu.
“Nampenda sana Ney kama rafiki, lakini tuna vipaumbele tofauti.”
Hapo awali Neymar alitumia misimu minne iliyosheheni mataji Camp Nou kati ya 2013 na 2017, akishinda mataji matatu mwaka 2015, kabla ya kufanya uhamisho wa rekodi ya dunia wa euro milioni 222 kwenda PSG.
Ameshinda orodha ya mataji ya Ligue I katika mji mkuu wa Ufaransa, lakini hajaweza kuisaidia PSG kushinda taji la kwanza la Ligi ya Mabingwa Ulaya licha ya kucheza pamoja na Messi na Kylian Mbappe kwa misimu miwili iliyopita.
Muda mwingi wa Neymar akiwa Paris amekuwa nje ya uwanja akiwa majeruhi, huku maradhi mbalimbali yakimfanya kucheza mechi 112 pekee za Ligue 1 ndani ya misimu sita kamili klabuni hapo.
Manchester United na Chelsea pia zimeonesha nia ya kumtaka Neymar.