Kocha Mkuu wa Simba SC, Mbrazili, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amefichukua mpaka sasa hana presha yoyote juu ya safu yake ya kiungo kutokana na ubora mkubwa unaonyeshwa na viungo wake wa kati, Mzamiru Yassin na Fabrice Ngoma hali inayopelekea kutapa ugumu wa chaguo la kwanza.

Robertinho ametoa kauli hiyo kutokana na ubora wa viungo hao katika eneo la kati kwa kuweza kuituliza timu na kuweza kutengeneza mashambulizi ambapo mpaka sasa Simba SC imefanikiwa kushinda mechi nne za mashindano zikiwemo mbili za Ligi Kuu Bara.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Robertinho alisema kuwa ubora mkubwa unaonyeshwa na safu yake ya kiungo cha kati kinapelekea kutokuwa na mchezaji mwenye nafasi ya uhakika kutokana na wote kuwa kwenye ubora unaofanana katika kutekeleza majukumu ya timu ndani ya uwanja.

“Timu ipo kwenye wakati mzuri kwa ajili ya mashindano ambayo yapo mbele yetu kutokana ukubwa wake, ukiangalia tuna Ligi ya Mabingwa Afrika, Super League, Kombę la FA pamoja na michuano ya Mapinduzi, lakini napata furaha zaidi kwa sababu karibu kila idara wachezaji wamekuwa wakionyesha ubora wa kiwango kikubwa ambacho kinachangia kupata matokeo mazuri.

Hakuna ambaye anaweza kusema anaweza kuwa na nafasi ya kudumu ndani ya timu yangu kwa sababu wote wamekuwa katika ubora mkubwa, angalia eneo la kati kuna Mzamiru, Ngoma pamoja na Sadio Kanoute, ambao wote wanaisadia timu kwa kutimiza majukumu yao kwa kila ambaye anayepata nafasi ya kucheza,” amesema Robertinho.

Rais Mnangagwa arejea tena madarakani
DC Mkuranga awashika pabaya wapiga dili