Jamii imeshauriwa kuachana na ngono kwa njia ya mdomo kwa kuwa inachangia maambukizi ya virusi vya Ukimwi (VVU).
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya DARE Dkt. Lilian Benjamin wakati akizungumza katika semina ya Wahariri na Waandishi wa Habari ambapo ameeleza kuwa ute unaopatikana chini ya fidhi na majimaji yaliyopo kwenye sehemu za siri za mwanamke vimethibitika kitaalamu kuwa vinaweza kuwa na VVU.
Dkt. Lilian ameeleza kuwa kufanya aina hiyo ya ngono kuna weza kuchangia maambukizi na maradhi mengine katika mwili.
Naye Ofisa Ufuatiliaji na Tathimini Tume ya Taifa ya Kuthibiti Ukimwi (TACAIDS) Nyangusi Laiser amesema kuwa majimaji yaliyopo mdooni yana weza kuwa na chembechembe za damu ikiwa kama mdomo unamichubuko ni rahisi kumuambukiza mwenzake VVU.
Aidha Laiser amebainisha kuwa vijana kati ya umri wa miaka 15 hadi 24 wanaongoza kwa maambikizi maoya ya VVU kwa asilimia 80.