Nchini Tanzania, mkoani Arusha wanafunzi 12 wamepewa ujauzito huku wengine wakiolewa kati ya mwezi January hadi April mwaka huu.
Taarifa hiyo inafuata baada uchunguzi uliofanywa na waandishi wa habari wa Msichana Initiative na Mimutie Women Organization,iliyothibitishwa na viongozi wa halmashauri ya wilaya Ngorongoro ambayo ilibaini wimbi la watoto kupata ujauzito.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri wilaya ya Ngorongoro Emanuael Sukums amesema kuna tatizo la wakazi wa ngorongoro kutothamini elimu hivyo kuwatoa watoto shule.
Ameongeza kuwa kuna baadhi ya wazazi wanashirikiana na watuhumiwa kujikinga na vyombo vya dola.
Taifa la tatu kwa kunyonga watu duniani, limefuta adhabu hiyo kwa watoto
Naye Mkurugenzi wa shirika la Mimuties , Rose Njilo ameomba serikali kuongeza ufuatiliaji kwa wanafunzi wa kike kwani hatua zisipochukuliwa nusu ya wanafunzi wa kike wa sekondari na msingi wanaweza wasirejee shuleni kwa kuolewa.
Ofisa maendeleo ya jamii wilayani Ngorongoro Benethez Bwilizo amesema wamepokea taarifa za wanafunzi wanne wa shule ya msingi na sita wa sekondari kupewa ujauzito katika kipindi hiki.