Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania ‘BFT’ limeweka hadharani ratiba ya Michuano ya wazi ya Ubingwa wa Taifa itakayoanza Mei 29, jijini Dar es salaam.
Taarifa iliyotumwa na kusainiwa na Katibu Mkuu wa BFT Makore Mashaga imeeleza kuwa, Michuano hiyo itaunguruma katika Ukumbi wa Manyara Park Tandale, kuanzia saa tatu asubihi.
Kabla ya kuanza Michuano hiyo Mapema Mei 29, kutakuwa na zoezi la Sports check entry ikifuatiwa na mkutano wa ufundi na kupanga ratiba.
“Mei 30 kuanzia saa mbili hadi saa tatu asubuhi Manyara park, tutakuwa na zoezi la kupima uzito na afya kwa mabondia wote watakaocheza siku hiyo na jioni kuanzia saa tisa alasiri tutakuwa na zoezi la ufunguzi rasimi wa mashindano na kuanza mashindano kwa hatua ya mtoani.”
“31/05/2023 saa mbili asubuhi hadi saa tatu tutakuwa na zoezi la kupima afya na uzito mabondia wote walio katika ratiba ya kucheza siku hiyo na kuanzia saa tisa alasiri tutaendelea na mashindano hatua ya robo fainali.”
“01/06/2023 kuanzia saa mbili hadi saa tatu tutaendelea na zoezi la kupima uzito na afya mabondia wote watakaokuwa kwenye ratiba ya kucheza siku hiyo na saa tisa jioni tutaendelea na mashindano kwa hatua ya nusu fainali”
“02/06/2023 kuanzia saa mbili hadi saa tatu kupima uzito kwa mabondia wote waliofika hatua ya fainali na saa kumi jioni kuendelea na mashindano hatua ya fainali na kufatia kutoa medali kwa mabondia mabingwa wa ubingwa wa taifa 2023.”
“Aidha tarehe 03/06/2023 tutakuwa na mkutano mkuu maalum wa Shirikisho la ngumi Tanzania utakaofanyika kuanzia saa tatu asubuhi katika ukumbi wa Manyara Park Tandale, Dar es salaam. Ajenda kuu ni marekebisho ya katiba ya Shirikisho.” Imeeleza taarifa ya BFT iliyosainiwa na Katibu Mkuu Makore Mashaga