Hatua ya Timu ya Taifa ya Argentina kutinga Fainali ya Copa America 2021, ni mtihani mkubwa kwa Nahodha na Mshambuliaji wa timu hiyo Lionel Messi.

Messi anakabiliwa na kiu ya mataji, kufuatia kikosi cha Argentina kushindwa kufikia lengo la kutwaa taji kwa kipindi kirefu, licha ya kucheza michezo ya mitatu ya Fainali wakiwa na Mshambuliaji huyo.

Mara mbili Argentina wakiwa na Lionel Messi walishindwa kutwaa taji la Copa America na mara moja wakakosa ubingwa wa dunia.

Fainali ya mwaka huu dhidi ya Brazil itakuwa ya nne kwa Argentina inayoongozwa na Messi kama Nahodha, acha tuangalie itakuwaje kwa upande wake, kwani amekuwa akijitahidi kadri ya Uwezo wake lakini anaishia patupu.

Rekodi ya Messi katika fainali za Copa America 2021, amecheza michezo 6, amefunga mabao 4 na ametoa pasi za mwisho (Assists) 5.

Timu ya taifa ya Argentina imefanikiwa kutinga fainali ya Copa América kwa kuifunga timu ya taifa ya Colombia kwa changamoto ya mikwaju ya penati 3-2, baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya kufungana 1-1.

Argentina itacheza fainali dhidi ya wenyeji Brazil walioiondosha Peru kwa kuifunga bao 1-0 usiku wa kuamkia jana Jumanne (Julai 06).

Mchezo wa fainali umepangwa kuchezwa usiku wa kuamkia Jumatatu (Julai 12) saa 10:00 Alfajiri.

Mzee Samatta: Morrison angetamba sana
Neymar: Mungu amejibu maombi yangu