Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Brazil Neymar Jr, amesema hana budi kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kukubali maombi yake.

Neymar amesema alifanya maombi ili Brazil ikutane na timu ya taifa ya Argentina kwenye mchezo Fainali wa Copa America 2021, na Mwenyezi Mungu amemkubalia Maombi yake.

Mshambuliaji huyo anaeitumikia klabu ya PSG ya Ufaransa, amesema anajua mashabiki wengi duniani walitamani kuiona Colombia ilicheza fainali dhidi ya Brazil, lakini kwake hakutaka iwe hivyo.

“Wengi walitamani tukutane na Colombia katika fainali, lakini mimi nilitamani tukutane na Argentina, kwa sababu inatakiwa tumfunge aliye bora.”

“Kwa hiyo Argentina wanakutana fainali na sisi Brazil tulio bora ukanda wa America na dunia nzima,” amesema Neymar

Timu ya taifa ya Argentina imefanikiwa kutinga fainali ya Copa América kwa kuifunga timu ya taifa ya Colombia kwa changamoto ya mikwaju ya penati 3-2, baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya kufungana 1-1.

Argentina itacheza fainali dhidi ya wenyeji Brazil walioiondosha Peru kwa kuifunga bao 1-0 usiku wa kuamkia jana Jumanne (Julai 06).

Mchezo wa fainali umepangwa kuchezwa usiku wa kuamkia Jumatatu (Julai 12) saa 10:00 Alfajiri.

Ni furaha kwa mashabiki, mtihani kwa Messi
Martinez aibeba Argentina Copa America 2021