Taarifa zinasema kuwa huenda klabu ya Young Africans ikamsajili Mlinda Lango Bora wa Ligi Kuu ya Mali, Diarra Djigui kwa makubaliano ya kuwa chaguo la kwanza kwenye kikosi cha Kocha Nasredine Nabi msimu wa 2021/22.
Djigui ambaye atatua Young Africans akitokea klabu ya Stade Malien ambao ni mabingwa wa nchini Mali, anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka miwili ndani ya klabu hiyo, iliyodhamiria kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Djigui mwenye umri wa miaka 26, alikuwa nahodha wa timu ya taifa ya Mali iliyoshiriki Fainali za Mataifa Bingwa Barani Afrika ‘CHAN 2020’, amependekezwa na kocha Nesreddine Nabi ambaye amekuwa akitafuta Mlinda Lango mwenye sifa anazozihitaji.
Kuwasili kwa Djigui, kutalazimisha kuondoka kwa Mlinda Lango mmoja ndani ya Young Africans kati ya Ramnadhan Kabwili ama Farouk Shikalo ambaye ni chaguo la kwanza kwa sasa.