Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa imeuchagua mji mkuu wa ufaransa, Paris, kuwa mwenyeji wa michuano ya Olimpiki ya mwaka 2024, na kuutunuku mji wa Los Angeles wa Marekani kuwa mwenyeji wa michuano hiyo kwa mwaka 2028 .
Mwezi uliopita, kamati hiyo ilifanya maamuzi ya kuwa Olimpiki mbili za majira ya joto zitatolewa kwa wakati mmoja, baada ya miji kadhaa kuahirisha zabuni zao kutokana na wasiwasi kuhusu ukubwa wa gharama na utata wa kuandaa moja ya matukio makubwa kama hayo ya michezo duniani.
Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amesema uchaguzi wa mji wa Paris kuwa mwenyeji wa michuano hiyo ni ishara ya kutambuliwa kwa mji na nchi, kitu ambacho kila Mfaransa anapaswa kusherehekea.