Msanii Nikki wa pili ameuponda mfumo mzima wa elimu Tanzania na kusema umeegemea upande mmoja na kupelekea watu wengine kukosa haki ya msingi ya kupata elimu hiyo.

Msanii uyo ameendelea kuuponda mchakato mzima unaotumika kuchuja kuwapata wasomi na kusema kuwa mchakato huo unamlazimu mwanafunzi kukariri mambo na si kuyaelewa.

Aidha ameeleza kuwa richa ya kuwa na malalamiko mengi juu ya wanafunzi kulega kuhudhuria shule hii ni kutokana na kukosa mfumo bora wa kuwapeleka watoto hao katika kutimiza ndoto  zao zaidi ya kukaririshwa kuhusu elimu.

Kwani hata walimu nao wamekuwa mstari wa mbele kusahau vipaji vingine na kuweka jitihada za kuviendeleza zaida ya kuwakaririsha kile ambacho wanaamini kitawafikisha malengo yao.

”Ukienda shuleni sasa hivi nikimuambia mwalimu anipe wanafunzi 10 wenye akili ataniletea anayejua hesabu, physics na masomo mengine lakini sitaletewa mwanafunzi anayejua kuchonga au anayejua muziki ‘so’ ikifika hapo unakuta mwanafunzi mwenyewe anaamua kufuata kile ambacho anaona anakiweza. Hivyo kwa mfumo huu hata wasanii wengi unakuta hawaendi shule” , amesema Nikki.

Ambapo ameeleza kuwa sio kwamba wasanii hawapendi kusoma, ila kinachotokea ni kuwa wanabaguliwa katika kile wanachokiamini kukipenda na kuwatimizia ndoto zao.

 

 

Ciro Immobile avunja rekodi ya Andriy Shevchenko
JPM atoa neno kuhusu hukumu ya kifo