Rapa kutoka kundi la Weusi, Nickson Simon ‘Nick wa pili’ amesema anaamini elimu yake ya shahada ya uzamili ‘masters’ na sasa anaendelea kuisaka shahada ya uzamivu ‘PHD’ itamsaidia kuinua zaidi ndoto zake na mafanikio katika muziki na maisha yake.
Mikakati yake ni kuwekeza elimu katika maisha na muziki kiujumla ili aweze kufika mbali zaidi na kutimiza malengo yake.
”Wasanii wanaotamani kurudi shule wawekeze shuleni, mimi nililenga kuwekeza katika elimu na nimefanikiwa na najua itanisaidia kwenye muziki na maisha yangu kiujumla, ndiyo maana muda mwingi nautumia kuangalia mbali zaidi juu ya elimu na muziki,” alieleza Nikki.
Wasanii wengi hujisahau hasa wakishaanza kushika pesa, hudhani maisha yameishia hapo vitu kama elimu hawatilii maanani,
Ikumbukwe kuwa muziki ni kazi ambayo ina muda wake, hasa hasa muziki wetu wa kizazi kipya yaani bongo flava, hivyo basi wasanii wawe makini sana kutambua umuhimu wa elimu wakiwa kwenye fani ya muziki hata baada ya kuachana na maswala ya muziki au sanaa kiujumla.
Wako api kina Mr nice, Juma nature, O-ten, Daz nundaz, Raha p, Sister p, Dataz na wakongwe wengine, hawasikiki tena kisanaa hata katika nyanja nyingine kama biashara, uchumi na siasa tofauti na wasanii wengine kama kina Professa Jay, Mr 2, na wasanii wengine ambao wamejikita katika siasa zaidi kutokana na elimu yao.
Inawezekana Diamond akatumika mfano kwa wasanii ambao hawataki kusoma wakiamini sanaa kama mkombozi.
La msingi ni kujifunza kwa yale yaliyowatokea wengi, ngekewa aliyoipata Diamond ni kitu kinachotokea kwa mtu mmoja kati ya mia.