Mtangazaji wa Shirika la Habari la Uingereza, BBC, Salim Kikeke, ambaye ni raia wa Tanzania ameonyesha kusikitishwa kwake na taarifa za watu wanaosema anaihujumu nchi ya Tanzania
kupitia ukurasa wake wa instagram Kikeke amesema kuwa watu hao wanania ya kumchafua wakisema anaidharau na kuihujumu Tanzania kwa kutoa habari zinazoididimiza .
“Nimesikitishwa sana na tuhuma zinazosambazwa mitandaoni dhidi yangu. Nataka kusema bayana kama Mtanzania, nawaheshimu watu wote nje na ndani ya Tanzania bila kujali jinsia umri au itikadi zao” aliandika Kikeke.
Hii inakuwa ni mara ya kwanza kwa Salim Kikeke ambae ni moja ya watangazaji wanaokubalika zaidi Tanzania na Afrika mashariki ,kuingia kwenye mvutano wa namna hii na baadhi ya watu wanaoamini hana uzalendo kwa Taifa lake.