Mtangazaji wa Shirika la Habari la Uingereza, BBC, Salim Kikeke, ambaye ni raia wa Tanzania ameonyesha kusikitishwa kwake na taarifa za watu wanaosema anaihujumu nchi ya Tanzania

kupitia ukurasa wake wa instagram Kikeke amesema kuwa watu hao wanania ya kumchafua wakisema anaidharau na kuihujumu Tanzania kwa kutoa habari zinazoididimiza .

“Nimesikitishwa sana na tuhuma zinazosambazwa mitandaoni dhidi yangu. Nataka kusema bayana kama Mtanzania, nawaheshimu watu wote nje na ndani ya Tanzania bila kujali jinsia umri au itikadi zao” aliandika Kikeke.

Hii inakuwa ni mara ya kwanza kwa  Salim Kikeke ambae ni moja ya  watangazaji wanaokubalika zaidi Tanzania na Afrika mashariki ,kuingia kwenye mvutano wa namna hii na baadhi ya watu wanaoamini hana uzalendo kwa Taifa lake.

Sio kila anayeenda kwenye mkutano ni mpiga kura - Lissu
Nyumba za ibada zisitumike kunadi sera

Comments

comments