Mwenyekiti wa Bodi ya Parole Tanzania, Augustino Lyatonga Mrema amesema kuwa yupo tayari kuendelea na kazi hiyo, endapo Rais Dkt. Magufuli atamteua tena.
 
Ameyasema hayo kupitia kipindi cha East Africa Drive cha East Africa Radio, ambapo ameelezea mpango wake wa kuwatoa wafungwa takribani 5000.
 
”Pamoja na kipindi changu kuisha lakini nipo tayari kuendelea endapo Rais Magufuli ataniteua tena na lengo ni kutimiza ndoto yangu ya kutoa wafungwa zaidi ya 5000”, amesema Mrema.
 
Aidha, mwanasiasa huyo nguli ameongeza kuwa Katika kipindi chake cha miaka mitatu kilichomalizika Julai 16, 2019, amefanikiwa kuwatoa wafungwa zaidi ya 600, ambapo amedai nia yake ilikuwa kuwatoa wafungwa 5000
 
Kwa upande mwingine Mrema ameiomba Wizara ya Mambo ya Ndani kupitia kwa Mawaziri wake ambao ni Kangi Lugola na Naibu wake Hamad Masauni, iharakishe michakato ya kuwatoa wafungwa wanaopendekezwa na Bodi ya Parole ili kupunguza msongamano wa wafungwa kwenye Magereza nchini.
 
Hata hivyo, Mrema aliyeteuliwa na Rais John Magufuli, kuongoza bodi hiyo Julai 16, 2016, hivyo Julai 16, 2019, alitimiza kipindi cha miaka mitatu cha kuongoza bodi hiyo.

Video: Makonda azindua soko la Madini jijini Dar, 'Tutawakomesha matapeli'
Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Julai 18, 2019