Kiongozi chama cha Economic Freedom Fighters (EFF), nchini Afrika Kusini, Julius Malema amesema ataipa silaha Urusi kwa sababu Moscow iko katika vita na ubeberu.

Malema ameyasema hayo wakati wa mahojiano na BBC mjini Johannesburg na kusisitiza kuwa Afrika Kusini ni mshirika wa Urusi na kwamba msimamo wa serikali ya ANC wa kutojihusisha na siasa unahusu vita vya Ukraine pekee.

Amesema, “nitaendeleza zaidi ya urafiki na Urusi na katika vita nitaungana na Urusi na nitaisambazia silaha,” alisema Malema na kudai EFF pia inataka Afrika Kusini kujiondoa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).

Hatua hiyo inatokan ana ICC kuoa hati ya kukamatwa kwa Vladimir Putin kwa madai ya uhalifu wa kivita lakini Malema ameahidi kuzuia jaribio lolote la kumkamata rais wa Urusi, iwapo atahudhuria mkutano wa kilele wa Brics wa mwezi ujao jijini Cape Town.

Wanawake 30 watekwa wakidaiwa kushindwa kulipa ushuru
Fedha za CAF Super League zaipa jeuri Simba SC