Dunia haiishi visa, lakini niseme tu kupata uhakika wa jambo ni vema zaidi kuliko kuwa na mashaka, maana wahenga walisema ‘haraka haraka haina baraka’ na pia wakaongeza kuwa ‘subira yavuta heri’ na msemo mwingine ni huu, ……. ‘majuto ni mjukuu’.

Nakumbuka Familia moja katika kijiji cha Doko-Nesenyi, kilichopo Kaunti Ndogo ya Kabwangasi, Wilaya ya Butebo, nchini Uganda iliwahi kukumbwa na mshtuko baada ya kuzika kimakosa maiti waliyokuwa wakidhani ni ya binti yao aliyefariki.

Kulikuwa na Jamaa mmoja anaitwa Michael Muyiyi, yeye alisema kwamba alisikia ripoti ya habari kwenye kituo kimoja cha redio chenye makao yake makuu mjini Jinja kwamba mwili wa msichana uliokuwa ukioza ambao maelezo yake yalilingana na bintiye, ulipatikana ukielea kando ya Ziwa Victoria Novemba 25, 2019.

Anasema, “Maelezo ya mwili na aina ya mavazi zililingana na binti yangu wa miaka 18, anayeitwa Winnie Nandudu, ambaye aliondoka nyumbani mwezi Agosti, sasa mimina kakake yangu Patrick tulisafiri tulisafiri hadi Hospitali ya Kawolo ya Wilayani Buikwe kuuchukua mwili huo.”

Kwanza ndugu hao wawili walifika katika Kituo cha Polisi cha Buikwe ambako kesi hiyo ilikuwa imesajiliwa kwa namba CRB 03/25/11/2019 na kulingana na ripoti ya uchunguzi wa maiti siku ya Novemba 26, 2019 [PM NO-334/2019], msichana huyo inadaiwa alikufa kutokana na kunyongwa au kukosa hewa.

Hapo Polisi wakapewa barua ya kibali iliyotiwa saini na afisa wa Polisi mwenye Namba 21772-D/SGT aliyejulikana kwa jina moja la Christmas kabla ya kuuchukua mwili huo.

Muyiyi anasema, “tulipoingia katika hospitali ya Kawolo, niliangalia sura na mwili wa msichana huyo na nikawa na shaka lakini kaka yangu alisema ndiye basi sikupinga hivyo tulinunua jeneza haraka na kurudisha mwili nyumbani kwa mazishi.”

Amesema, ” Maajabu yakaanza kwani siku kadhaa baada ya mazishi, Nandudu alimpigia simu mama yake … sote tuliogopa kwa sababu tulikuwa tumetoka kuuzika mwili wake maana hatukuamini kwamba binti yetu bado yuko hai hapo tukashauriana na tulisafiri hadi Kampala ambako tulikutana naye.” anasimulia Muyiyi.

Mwisho kabisa, wakiwa njiani kutoka Kampala, inasemekana walikwenda kituo cha polisi cha Kawolo kueleza mkanganyiko huo na jinsi walivyoishia kuzika mtu asiyefaa lakini wakaambiwa hakuna mtu mwingine aliyewahi kuudai mwili huo.

AFCON 2027: Kenya kuboresha viwanja vinane
Uhusiano Tanzania, Afrika Kusini upo imara - Meja Jen. Milanzi