Serikali imetoa kiasi cha Shilingi Bilioni 5.6 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa skimu ya umwagiliaji katika Kijiji cha Kongogo, Kata ya Babayu, Tarafa ya Mundemu yenye ukubwa wa hekta 220.

Hayo yamebainishwa na Meneja wa Mradi toka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Raphael Laizer wakati akiwasilisha taarifa ya hali ya utekelezaji wa ujenzi wa bwawa hilo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule, katika eneo la mradi na kusema ujenzi wa skimu hiyo unaendelea na uko katika hatua za awali.

Akizungumza na wakazi wa eneo hilo mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa skimu hiyo ya umwagiliaji, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amesema azma ya Serikali ni kuhakikisha nchi inakuwa na kilimo cha kisasa kwa kulima mara mbili mpaka tatu kwa mwaka, kuhamasisha shughuli za uvuvi na mifugo bila kuathiri mazingira.

Amesema, “Kilimo cha uhakika duniani kote ni kilimo cha umwagiliaji, kilimo kinachowezesha wananchi kulima mara mbili hadi tatu kwa mwaka, maono ya Serikali ni kuhakikisha nchi ya Tanzania inakuwa miongoni mwa nchi nyingine duniani katika kulisha dunia kwa kusambaza chakula ndani na nje ya nchi.”

Mayele: Wachezaji Azam FC wanakamia mechi
Sakata la ubaguzi wa rangi La Liga