Mshambuliaji wa Klabu Bingwa Tanzania Bara Young Africans na Kinara wa mabao katika Ligi hiyo, Kombe la Shirikisho Afrika Fiston Mayele amesema mchezo wa Fainali Kombe la Shirikisho Tanzania Bara (ASFC) utakuwa mgumu.

Mshambuliaji huyo jana Jumapili (Mei 21) alifunga bao la ushindi dhidi ya Singida Big Stars na kuipeleka Young Africans Fainali ya ASFC ambapo watacheza dhidi ya Azam FC iliyoindoa Simba SC mapema mwezi huu.

Mayele amesema mchezo wa Fainali ambao utapigwa jijini Tanga katika Uwanja wa CCM Mkwakwani watakayokutana na Azam FC utakuwa mgumu kwa sababu timu hiyo yenye maskani yake Azam Complex Chamazi, imekuwa inakamia timu kubwa za Simba SC na Young Africans.

Mayele amesema wachezaji wa Azam FC wamekuwa waking’aa wanapocheza mechi dhidi ya Simba SC na Young Africans tofauti na wakicheza na timu nyingine za Ligi Kuu Tanzania Bara.

“Itakuwa mechi ngumu dhidi ya Azam FC ambao huwa wana tabia ya kukamia katika mechi kubwa.Ukitazama mechi zao dhidi ya timu za kawaida ni tofauti kabisa dhidi ya Simba SC na Young Africans , lakini tunaamini tutashinda hiyo mechi na huu kwangu ndiyo msimu bora tangu nimeanza kucheza soka la ushindani.”

“Huko nyuma katika mashindano ya kimataifa nilikuwa nafunga mabao mawili au matatu” amesema MShambuliaji kuyo kutoka DR Congo

CCM yatia mkono sakata la mgomo Kariakoo
Mabilioni kutumika ukalimishaji skimu ya umwagiliaji