Zaidi ya Wasomali milioni 1 wamesambaratika maeneo tofauti kutokana na hali ya ukame, na wengine Zaidi ya 213,000 wanakabiliwa na tishio kubwa la maisha kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kutokuwa na uhakika wa chakula.

Hayo yamebainika baada ya Mratibu mkuu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Martin Griffiths kuanza ziara nchini Somalia kushuhudia hali halisi ya njaa na kutathimini mahitaji ya walioathirika na hatua zinazochukuliwa kuwasaidia.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada yad harira (OCHA), karibu nusu ya Wasomali wote wanaokadiriwa kuwa watu milioni 7.8 wameathirika na ukame mkali kuwahi kushuhudiwa kwa miongo minne na katika miezi ijayo watakabiliwa na msimu wa tano bila mvua.

Hali ya ukame iliyosababisha ukosefu wa maji na chakula nchini Somalia. Picha na UN.

OCHA imesema, “Kuna hatari kubwa ya baa la njaa endapo uzalishaji wa mazao na mifugo utafeli. bei ya chakula inaendelea kupanda, na wale wenyeuhitaji zaidi hawapati msaada.”

Mashirika ya misaada yaliyoko nchini humo yanafanya kila wawezalo kuokoa maisha na riziki za waathirika na yanasema kuwa “Hadi kufikia mwisho wa Julai, walikuwa wametoa msaada kwa watu milioni 5.3.”

Mratibu huyo wa misaada ya dharura Griffiths, aanatarajia kukutana na jamii zilizoathirika, maafisa wa serikali na mashirika wadau na pia atakagua juhudi za pamoja za kuongeza haraka operesheni za misaada na kujadili hatua zilizopigwa na changamoto.

Biden alia na Trump mporomoko wa maadili
Wahujumu vyanzo vya Maji mikononi mwa Sheria