Umoja wa Mataifa (UN), umesema takriban raia 50 waliuawa katika operesheni ya wanajeshi wa Mali walioandamana na “wanajeshi wa kigeni” mwezi Aprili 2022 ikiwa ni kati ya jumla ya raia 96 waliouawa katika robo ya pili ya mwaka ya operesheni za Kijeshi.

Aprili 19, 2022 katika mji wa kati wa Hombori, baada ya kilipuzi kilichoboreshwa kulipuliwa wakati msafara wa Mali ukipita, vikosi vya Mali, vikiambatana na “wanajeshi wa kigeni, walifanya msako katika eneo hilo ambapo raia 50 wakiwemo wanawake na watoto waliuawa na wengine zaidi ya 500 kukamatwa.

UNMISMA, haikutoa maelezo yoyote kuhusu wapiganaji hao wa kigeni ambapo Nchi kadhaa za Magharibi zinaishutumu Serikali ya kijeshi iliyo madarakani huko Bamako tangu 2020, kwa kuajiri huduma za kampuni ya usalama ya Urusi ya Wagner.

Wanajeshi wa Mali wakiongea na Mama mmoja nchini humo. Picha na Reuters.

Hta hivyo, Junta inakanusha madai hayo na kusema uwepo wa wakufunzi wa jeshi la Urusi ni ushirikiano wa kijeshi wa muda mrefu kati ya mataifa hayo mawili ambayo yamekuwa yakifanya kazi pamoja.

Hata hivyo, tangu mwaka wa 2021, Jeshi la Mali limeachana na mshirika wake wa zamani wa Ufaransa, ambaye amekamilisha uondoaji wake wa kijeshi kutoka Mali baada ya uhusika wa miaka tisa.

Jeshi la Ufaransa, lilisema mwezi Aprili kwamba lilirekodi na kutoa picha za kile ilichodai kuwa mamluki wa Urusi wakizika miili karibu na kambi ya kaskazini ya Gossi, ambayo jeshi la Ufaransa lilijiondoa hivi karibuni. Kusudi lilikuwa kuwashtaki Wafaransa kwa kuacha kaburi la watu wengi nyuma.

Wanajeshi wakijadiliana jambo na Raia. Picha na hrw.org

Minusma alisema imefungua uchunguzi. Ilisema miili iliyozikwa Gossi ilisafirishwa hadi eneo hilo mnamo Aprili 20, siku moja baada ya Wafaransa kukabidhi kambi ya Gossi kwa Wamali, na “ilitoka Hombori.

Dejan atoa ahadi nzito Simba SC
Sudan na Marekani 'zaoneshana tabasamu' baada ya miaka 25