Licha ya utajiri wa urithi wa utamanduni, na mchango mkubwa unaotolewa na watu wenye asili ya Afrika katika jamii, bado wanakabiliwa na ubaguzi ulio ota mizizi kimfumo hasa kwa mataifa yaliyoendelea barani Ulaya.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya watu wenye asili ya Afrika yanayofanyika kwa mwaka wa pili tangu kuanza kwa maadhimisho hayo mwaka 2020.

Amesema, mwezi Desemba mwaka huu (2022), kutafanyika kikao cha kwanza cha Jukwaa la Kudumu la Watu Wenye Asili ya Kiafrika na kuhimiza watu wote kujiandaa kushiriki na kusukuma mbele kazi ya Jukwaa.

Jamii ya watu weusi. Picha kwa hisani.

“Duniani kote, mamilioni ya watu wenye asili ya Kiafrika bado wanashuhudia ubaguzi wa rangi uliokita mizizi na wa kimfumo na ndiyo maana Umoja wa Mataifa unaendelea kutoa wito wa kuheshimiwa haki za kibinadamu na uhuru wa kimsingi,” amesema Guterres.

Aidha, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limeomba kuwepo na kikosi kazi kitakacho simamia utekelezwaji kwa Ufanisi wa Azimio la Durban na Mpango wa Utekelezaji, kikosi kazi hicho kitaandaa rasimu ya tamko la Umoja wa Mataifa kuhusu kukuza na kuheshimu kikamilifu haki za binadamu za watu wenye asili ya Afrika.

Amesisitiza kuwa jukwaa litachangia kazi hii muhimu sana na kwamba, “ni muhimu kwa pamoja tuendelee kuongea kwa sauti kubwa na bila kukosa dhidi ya dhana yoyote ya ubaguzi wa rangi na kwamba tufanye kazi bila kuchoka ili kukomboa jamii zote kutoka kwa balaa ya ubaguzi wa rangi.”

Dkt. Mabula: Wananchi hawamudu gharama za nyumba
LAAC:Biharamulo hawakuwa tayari kukaguliwa