Serikali inatarajia kuchukua hatua dhidi ya kampuni zinazoleta migogoro kwa wananchi kwa kuwapimia watu vipande vidogo vidogo vya ardhi isiyopimwa, bila kujali suala la mipango miji na athari zinazoweza kujitokeza hapo baadaye.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula wakati akifungua Mkutano wa siku mbili wa Wadau wa Sekta ya milki Tanzania, ulioanza hii leo Septemba mosi, 2022 jijini Dar es Salaam.

Amesema, kampuni hizo zimekuwa na tabia ya kupima ardhi kisha kuwaambia wananchi waende ofisi za ardhi ili waweze kupimia hali wakijua ni makosa kisheria na kutoa onyo kwa wale wote wanaohusika kuacha tabia hiyo mara moja.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula.

“Mpimaji yeyote atakayepitisha viwanja vya mita 300 au 500 atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria kuanzia leo Sept. Mosi 2022 kwani hatua hiyo inawafanya wananchi kushindwa kufanya mipango yao kwa kukosa eneo stahiki linalotambulika kiukubwa kwa mijibu wa taratibu,” amefafanua Dkt. Mabula.

Aidha ameongeza kuwa, kitaaluma hakuna viwanja vya nna hiyo na wala havikubaliki na vinaaibisha taaluma ya mipango miji kutokana na tamaa ya baadhi ya watu ambao hujichukulia maamuzi bila kujali athari zinazoweza kujitokeza.

Kufuatia hatua hiyo, Waziri Mabula amezielekeza bodi ya usajili mipango miji na ile ya usajili wa uthamini kufanya tathmini na kuchukua hatua na makampuni ya upimaji au mtu anayepima vipande vya ardhi waache haraka na warudishe fedha za wananchi na kuwataka wananchi kupata taarifa au maelekezo na ushauri kwa ofisi za ardi kabla hawajanunua ardhi husika.

Baadhi ya Washiriki wa Mkutano wa siku mbili wa Wadau wa Sekta ya milki Tanzania, ulioanza hii leo Septemba mosi, 2022 jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo, amebainisha kuwa, maeneo ya makazi yanahitaji kupimwa kitaalamu na kuangalia uwezekano wa upatikanaji wa huduma za kijamii na si holela kama wafanyavyo baadhi ya watu ambao si waaminifu wakiwemo na madalali ambao sheria yao ipo jikoni.

Habari kuu kwenye magazeti ya leo September 2, 2022     
Kenya: Raila hapaswi kuilaumu IEBC kufeli kwa Mawakala - Gumbo