Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amerejea nchini akitokea nchini Tunisia ambako alimwakilisha Rais, Samia Suluhu Hassan, katika Mkutano wa nane wa Kimataifa wa Wakuu wa nchi na Serikali unaohusu ushirikiano baina ya Japan na Afrika TICAD.

Majaliwa, amerejea hii leo Jumatano Agosti 31, 2022 ambapo akiwa katika mkutano huo uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali, aliwasilisha miradi minane ya maendeleo yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 1.334.

Miradi hiyo, ni pamoja na ukarabati wa barabara ya Morogoro – Dodoma kwa kiwango cha Lami, Mradi wa umwagiliaji katika bonde la ziwa Victoria na Mradi wa kusambaza maji Lugoda (Mufindi).

Mradi mwingine ni ule wa kujenga uwezo wa kituo cha utafiti cha ufugaji wa samaki Dar es Salaam, Bandari ya kisasa ya uvuvi, kuanzisha maabara ya kuthibitisha ubora kwenye sekta ya uvuvi na ukarabati wa bandari ya uvuvi ya wete pamoja na ujenzi wa njia ya umeme ya Somanga – Fungu, Mkuranga.

Habari kuu kwenye magazeti ya leo September 1, 2022    
Tanzania 'mstari wa mbele' maendeleo ya jamii