Rais wa Shirikisho la Soka Nchini Ufaransa (FFF), Noël Yves Marie Le Graët (81) ambaye angebaki Madarakani hadi 2024 amejiuzulu baada ya tuhuma za unyanyasaji wa kingono huku ikibainika kuwa kuna ‘uchafu’ ndani ya FFF.
Kabla ya kuchukua uamuzi huo kiongozi huyo alijiweka pembeni kwa muda wakati Serikali ikifanya uchunguzi wa ofisi yake baada ya tuhuma mbalimbali, sasa amechukua maamuzi hayo baada ya ripoti kuelezea kuwa hana sifa za kuendelea kuwa kiongozi.
Mara zote Le Graet amekuwa akikanusha kuwa hana makosa, upande wa pili alipata presha kubwa ya kujiuzulu baada ya kumsema vibaya nguli wa Ufaransa, Zinedine Zidane kuhusu nafasi yake ya kuifundisha timu ya Taifa hilo ingawa baadaye aliomba radhi.
Le Graët alizwaliwa Desemba 25 mwaka 1941, amebobea katika Biashara, Siasa na Soka.
Le Graët alichaguliwa kuwa Rais wa Shirikisho la Soka nchini Ufaransa ‘FFF’ kuanzia mwaka 2011 hadi 2023. Kabla ya hapo alikuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho hilo kuanzi mwaka 2005.