Kikosi cha African Sports kimewasili jijini Dar es salaam, tayari kwa mchezo wa Hatua ya 16 Bora, Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ dhidi ya Simba SC.

Mchezo huo umepangwa kupigwa kesho Alhamis (Machi 02), katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam, kuanzia saa kumi jioni.

Msafara Africans Sports FC umewasili jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo ukiwa na watu 18, ambapo Wachezaji ni 15 na Viongozi wa Benchi la ufundi watatu.

Uchache wa watu waliojumuika kwenye msafara huo, unatajwa umetokana na hali ya kiuchumi inayoikabili Africans Sports, inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Tanzania ‘Championship’ ikishika nafasi ya tisa kwa kuwa na alama 21.

African Sports ilitinga Hatua ya 16 Bora ASFC, baada ya kuifunga New Dundee kwa changamoto ya Mikwaju ya Penati 4-2, huku Simba SC ikiifunga Coastal Union 1-0.

Julio aitaka Azam FC leo, kesho
Petit aionya Arsenal kwa Mbappe