Kiungo wa zamani wa Arsenal Emmanuel Petit amewataka The Gunners kuepuka kumsajili Mchezaji wa Paris Saint-Germain, Kylian Mbappe.

Mbappe amejidhihirisha kuwa mmoja wa wachezaji bora zaidi duniani katika miaka ya hivi karibuni, akifunga mabao 200 na kutoa asisti 95 zaidi katika mechi 246 pekee za PSG.

Real Madrid imekuwa ikitajwa kama mahali pazuri pa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa na Petit amewaambia The Gunners kusahau kuhusu kujaribu kumsajili Mbappe.

“Arsenal haipaswi kumnunua Kylian Mbappe. klabu pekee inayoweza kumshawishi Mbappe kwa sasa, na pengine milele, ni Real Madrid.” amesema Petit

Mbappe amekuwa akitajwa kuwaniwa na klabu kadhaa Barani Ulaya kutokana na kuwa na uwezo mkubwa wa kupambana na kufunga mabao, lakini hadi sasa Klabu yake ya PSG haijatoa taarifa za kutarajiwa kumuweka sokoni.

Africans Sports yawasili Dar es salaam kinyonge
Erasto Nyoni: Nimewasaida kwa kuwatia moyo