Nahodha wa Timu ya Soka ya Taifa ya Wasichana wa umri chini ya miaka 17 (Serengeti Girls), Noela Luhala, amesema wanamshukuru Mungu kwa matokeo mazuri wanayopata na kesho Jumamosi (Oktoba 22) wataendelea kupambana ili kupata ushindi.

Serengeti Girls inatarajia kuivaa Colombia katika mchezo wa hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Dunia utakayochezwa kesho Jumamosi (Oktoba 22) kwenye Uwanja wa Pandit Jawaharial Nehru, Goa.
Luhala amesema wanafahamu wameingia hatua ya mtoano, hivyo watacheza kwa kiwango cha juu kwa malengo ya kusaka ushindi.

“Sisi kwetu tunaifananisha na mechi ya fainali, ukiingia fainali basi mawazo yanakupeleka katika ushindi, ndio tutakavyoingia, kwetu kila mechi ni muhimu, tunaziheshimu timu zote tunazokutana nazo, tunaamini huu ni mwaka wetu, tunataka kuendelea kumpa furaha Rais, Samia Suluhu Hassan,” nahodha huyo amesema.

Robo Fainali nyingine ya michuano hiyo itakayochezwa leo Ijumaa (Oktoba 21), itawakutanisha Marekani dhidi ya Nigeria.

Maandalizi mrithi wa Waziri Mkuu yaanza
Kocha Shime autaka mchezo wa Colombia