Kiungo kutoka nchini Burundi na Klabu ya Simba, Saidi Ntibanzokiza ‘Saido’ ameandika rekodi yake kimataifa kwa kuwa nyota wa kwanza kuonyeshwa kadi ya njano kwenye hatua ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa upande wa Simba SC, dakika mbili akiwa uwanjani.
Simba SC juzi Jumamosi (Septemba 16) ilikuwa na kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos ambapo Ntibanzokiza alianzia benchi.
Alipopewa nafasi ya kuingia dakika ya 60 akichukua mikoba ya Willy Onana dakika ya 62 alicheza faulo iliyopelekea mwamuzi kumuonyesha kadi ya njano ikiwa ni ya kwanza kwake na Simba SC kiujumla katika anga la kimataifa msimu wa 2023/24.
Mbali na kuwa nyota wa kwanza kuonyeshwa kadi ya njano Ntibanzokiza alikosa nafasi ya dhahabu kupachika bao ilikuwa dakika ya 65.
Ni shuhuda ubao wa Levy Mwanawasa, Zambia ukisoma Power Dynamo 2-2 Simba SC huku mabao yote ya Simba SC yakifungwa na Clatous Chama.
Kete ya pili inatarajiwa kuchezwa Oktoba Mosi, Uwanja wa Azam Complex ambapo mshindi wa jumla atakata tiketi ya kusonga hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.