Afisa Mhamasishaji wa Young Africans Antonio Nugaz ametupa dongo kuelekea mchezo wa Jumamosi (Julai 03) dhidi Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC.

Nugaz ametupa dongo hilo kama sehemu ya utani uliodumu kwa miaka mingi baina ya klabu hizo za Kariakoo, ambapo amesisitiza siku zote wamekua wakicheza michezo yao pasina kudhulumu.

Amesema anaamini wana kikosi kizuri kitakachoikabili vizuri Simba SC na mwisho wa dakika 90 wataondoka Uwanja wa Mkapa wakiwa na kichezo cha ushindi.

“Sisi hatudhurumu mechi zetu, sisi tunashinda kwa haki na bila dhurumu na bila ujanja ujanja, wambie waje uwanjani watakupa majibu na wasilete ujanja ujanja.” Amesema Nugaz.

Simba SC inayoongoza msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kufikisha alama 73, Jumamosi (Julai 03) itakuwa mwenyeji wa Young Africans iliyo nafasi ya pili kwa kumiliki alama 67, huku Azam FC ikishika nafasi ya tatu kwa kuwa na alama 63.

Wakati huo huo Shirikisho la Soka Tanzania Bara (TFF) limetangaza majina ya waamuzi watakaochezesha mpambano wa Jumamosi (Julai 03), Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Polisi Tanzania yasisitiza alama 6
Dkt. Mpango atoa ahadi za Tanzania katika jukwaa la kizazi chenye usawa