Harry Kane ni miongoni mwa wachezaji katika ligi ya Uingereza aliyeteuliwa kuwania tuzo ya mchezaji bora wa Fifa mwaka 2017 .
Aidha, mshambuliaji huyo wa Tottenham anakabiliwa na upinzani mkubwa kutoka kwa wachezaji wenzake wa ligi kuu ya Englanda akiwamo Alexi Sanchez wa Arsenal, kiungo wa kati wa Chelsea Eden Hazard na N’Golo Kante katika orodha ya wachezaji 24.
Hispania imetoa wachezaji wakali wanaotikisa ligi hiyo na dunia kwa ujumla ambao ni mshindi wa tuzo za mwaka jana, Cristiano Ronaldo pamoja na Lionel Messi wa Bareclona, huku ligi ya Ufaransa ikitoa nyota mmoja wa PSG Neymar.
Hata hivyo, wengine ni Zlatan Ibrahimovic ambaye kwa mara ya mwisho aliichezea Manchester United ambapo imeelezwa kuwa upigaji kura utakamilika tarehe 7 mwezi Septemba na washindi watatangazwa katika sherehe ya kutoa zawadi tarehe 23 mwezi Oktoba mwaka huu.