Kiongozi wa Chama cha upinzani nchini Zambia UPND, Hakainde Hichilema ameachiliwa huru mara baada ya kiongozi wa mashtaka nchini humo, Lillian Siyunyi kuyaondoa mashitaka ya uhaini dhidi yake.

Mahakama kuu nchini humo imeifuta kesi hiyo ya uhaini dhidi ya kiongozi wa upinzani, Hakainde Hichilema na kumuachia huru na wenzake watano ambao walikuwa wanakabiliwa na mashtaka hayo.

Aidha, Msemaji rasmi wa chama cha upinzani cha National Restoration Party, Narep Bwalya Nondo, amesifu maamuzi ya mahakama hiyo lakini huku akisema bado anahofu ya kukamatwa tena kwa kiongozi huyo.

“Tunayofuraha kubwa mwenzetu ameachiliwa huru kutoka jela, lakini tunahuzunika kuwa hana uhuru kwa sababu Serikali halimruhusu mshukiwa yeyote wa uhalifu kuwa na uhuru kamili, anaweza kukamatwa tena kwa mashtaka hayo hayo na arudishwe rumande.”amesema Nondo.

Hata hivyo, Hichilema alikamatwa mwezi Aprili mwaka huu na kushtakiwa kwa kosa la uhaini kufuatia kugoma kupisha msafara wa Raiswa nchi hiyo,  Edgar Lungu hivyo kupelekea kukamatwa kwa kosa la kuhatarisha maisha ya Rais.

Museveni agonga mwamba kubadili Katiba
Nyota wa La Liga uso kwa uso na wa EPL tuzo za mchezaji bora