Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, January Makamba amewataka wakazi wa wilaya ya Nzega kuwa wakali kwa rasilimali zao na kuhakikisha mazingira kwa ujumla wake yanatunzwa kwa sheria kali zaidi.
Ameyasema hayo mara baada ya kufanya ziara na kupokea taarifa kutoka kwa mkuu wa wilaya hiyo, Godfrey Ngukuwa kuhusu uharibifu wa mazingira.
Aidha, Makamba ameagiza kufanyika kwa operesheni kali na kuwachukulia hatua wale wote wanaojihusisha na uharibifu huo.
“Ndugu zangu sina budi kuwakumbusha kuwa siku hizi kuna wakimbizi wa Mazingira, watu wanaharibu mazingira katika maeneo yao na kuhamia maeneo mengine, jitihada za maendeleo zote hazitakuwa na maana kama hatutatunza mazingira,” amesema Makamba
Hata hivyo, Makamba amewaeleza wakazi wa Vijiji vya Ngukumo na Mwambaha kuwa na uhifadhi wenye tija ni ule ambao wananchi wako tayari kushiriki kwa nguvu zote katika kuunga mkono shughuli za maendeleo.
-
Makamba aagiza uanzishwaji wa kamati za mazingira
-
NACTE yatoa ufafanuzi ucheleweshaji wa namba ya uhakiki AVN
-
Video: Mimi napambana kwaajili ya Rais Dkt. Magufuli tu- Musiba