Rais wa Marekani, Barack Obama ameendelea kuonesha jinsi anavyomkubali rapa Kendrick Lamar na kumuweka juu ya rapa Drake.

Katika mahojiano maalum aliyofanya na YouTube, Ijumaa wiki hii, Obama hakuficha kura yake pale alipotakiwa kutengua kitendawili cha ‘nani mkali kati ya Kendrick na Drake.

“Ningemchagua Kendrick,” alisema Obama. “Nadhani Drake ni msanii bora, lakini Kendrick… mashairi yake, album yake ya mwisho (To Pimp a Butterfly) ilikuwa bora, albam bora zaidi kwa mwaka jana nadhani,” Obama aliitetea kura yake.

Hivi karibuni, Obana alimualika Kendrick Ikulu ya Marekani kwa lengo la kumpongeza kwa wimbo wake ‘How Much a Dollar Cost’ ambao aliutaja kuwa wimbo alioupenda zaidi kwa mwaka 2015.

Angalia hapa mahojiano aliyofanya na YouTube:

Tanzia: Mwandishi wa 'Ngoswe, Penzi Kitovu cha Uzembe' afariki
Bavicha wataka Msajili aifute CCM, la Sivyo watafanya hili