Chama cha upinzani cha Labour nchini Nigeria kinatarajia kupinga ushindi wa Bola Tinubu wa chama tawala cha APC katika Uchaguzi wa Rais.

Peter Obi wa chama cha Labour ameshika nafasi ya tatu katika kura zilizopigwa Jumamosi. Upinzani unasema matokeo yalichakachuliwa na wanataka warudie kupiga kura upya.

Huku kukiwa na 28% tu ya wapiga kura walioshiriki kupiga kura Nigeria na wengine kushindwa kupiga kuwara kutokana na sababu ya ubovu wa mashine.

Asiwaju Bola Tinubu wa Chama cha All Progressives Congress amepata kura 37%, ikiwa ni idadi ndogo ya ushindi tofauti na marais waliopita wa Nigeria.

Waangalizi wa uchaguzi wa Umoja wa Ulaya walisema kumekuwa na mapungufu makubwa katika mchakato wa uchaguzi, na kuongeza kuwa kumekuwa na ununuzi wa kura lakini ilikuwa mapema mno kusema jinsi hali hiyo ilivyoenea.

Chama cha wafanyakazi cha Nigeria kinachoongozwa na mgombea urais Peter Obi kitawasilisha pingamizi la kisheria dhidi ya kuchaguliwa kwa rais mteule, Bola Tinubu, mgombea makamu wa rais wa chama hicho alisema.

Zoran Maki afunguka kilichomuondoa Simba SC
Mama Feisal avunja ukimya, aitaka TFF kutenda haki