Asiwaju Bola Tinubu, mgombea urais wa chama cha  All Progressives Congress, anatarajiwa kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais wa 2023 baada ya kupata kura 8,805,420 za uchaguzi wa Februari 25 katika matokeo yanayoendelwa kutangazwa.

Atiku Abubakar wa chama cha Peoples Democratic Party ndiye mpinzani wa karibu zaidi wa Tinubu, na kulingana na hesabu ya kura zilizotangazwa hadharani na maafisa wa uchaguzi kutoka majimbo 36 na Federal Capital Territory huko Abuja, Tinubu alikuwa mbele kwa si chini ya kura  milioni 1.8.

Asiwaju Bola Tinubu, mgombea urais wa chama tawala cha  All Progressives Congress – APC. Picha ya Nigeria Today.

Atiku, ambaye anaweza kuwa mshindi wa wa pili, amepata kura 6,984,290 huku mgombea wa Labour Party, Peter Obi, akiwa wa tatu kwa kupatq kura 6,093,962 na  watatu hao walishinda katika majimbo 12 kila moja.

Huko Kusini-Magharibi, ingawa Tinubu alipoteza Jimbo la Lagos, lililochukuliwa kuwa ngome yake yenye nguvu zaidi, kwa mgombea wa LP na Jimbo la Osun kwa mwenzake wa PDP, mzee huyo wa miaka 70 alishinda katika Jimbo la Oyo kwa kura 449,884, Ondo 369,924, Ekiti 201,494 na Ogun 341,554.

Tanzania, WB zasaini mkopo nafuu, msaada Trilioni 1.333
Waandamana kupinga Wachina kuuza bidhaa bei ya kutupa