Kiongozi waChama cha upinzani nchini Kenya Raila Odinga amesema anaunga mkono wito wa rais wa nchi hiyo, Uhuru Kenyatta wa kutaka rais ajae atoke katika jamii tofauti amabyo haijawahi kuongoza.
Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC news wakati akizungumza katika kikundi cha vijana nchini Kenya Raila amesema urais ni swala tata na nchi hiyo ni nchi yenye makabila mengi, hivyo ni lazima makabila hayo yaweze kuongoza nchi hiyo.
”Kama mnavyofahamau Kenya ni jamii yenye makabila mengi, na kutokana na hili tunalichukulia kwa umakaini kutokana na tofauti za kikabila amabzo tunazo katika nchi yetu” amesema Raila.
Kauli ya Odinga inatokana na msimamao wa Rais Uhuru Kenyatta kuibua mjadala katika mitandao ya kijamii nchini humo pale aliposema ”Ni makabila mawili tuu amabyo yameingoza Kenya tangu ipate Uhuru wake”.
Raila Odinga ameongeza kuwa ” huenda umefikia wakati kwa makabila mengine amabyo hayajawahi kuongoza kenya nayo kuongoza.
Hata hivyo akiunga makono kauli ya Rais Kenyatta, Raila amesema haoni madhara yoyote kama urais utakuwa ni wa zamu, hususa ni pale uteuzi unapofanywa na rais anayependelea watu kutoka makabila au jamii nyingine.