Kocha wa Timu ya Uganda iliyowasili nchini Japan kushiriki mashindano ya Olympic amebainika kuwa na virusi vya corona (covid-19).
Maafisa wa Serikali ya Japan wametoa taarifa hiyo kwa umma, ambapo Rais wa Kamati ya Olympic ya Uganda, Donald Rukare amesema kocha huyo hajaonesha dalili zozote za kuwa na corona.
Bado haijafahamika wazi kama kocha huyo ataruhusiwa kuendelea kushiriki mashindano hayo akisalia nchini humo au atarejeshwa nchini Uganda.
Aidha, Rukare amesema kuwa msafara mzima wa wanamichezo na maafisa wa Uganda waliongia Japan, ikiwa ni pamoja na wanamichezo 26 na wafanyakazi 30, walipatiwa dozi kamili ya chanjo ya corona aina ya AstraZeneca.
Rukare amefafanua kuwa wengi kati yao walipata chanjo hiyo mwezi huu ikiwa ni miezi mitatu baada ya kupata dozi ya kwanza.
Wanamichezo wengine wamepimwa na hawakuwa na covid-19; wamepelekwa kwenye jiji la Izumisano. Taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Jiji la Izumisano imeeleza kuwa wanamichoezo hao watakuwa wanapimwa kila siku.