Klabu ya Manchester United imepanga kumuuza kwa kiasi kikubwa cha fedha kiungo wao kutoka Ufaransa Paul Pogba, ambaye kwa sasa anawika na timu yake ya taifa kwenye michuano ya UEFA Euro 2020, inayoendelea katika miji mbalimbali Barani Ulaya.

Manchester United imepanga kumuuza kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28, kwa kiasi cha Pauni milioni 104, katika kipindi hiki cha dirisha kubwa la usajili.

Kwa mujibu wa gazeti la The Sun, Manchester United wapo tayari kumuuza kiungo huyo, kufuatia klabu ya PSG ya Ufaransa kuonesha nia ya kutaka kumsajili, na wanajipanga kuwasilisha ofa huko Old Trafford mjini Manchester, England.

Gazeti hilo limetoa ufafanuzi kuwa, kiasi cha fedha ambacho kitapatikana baada ya mauzo ya kiungo huyo, kitatumika kwenye ushawishi wa kumsajili beki kutoka nchini Ufaransa Raphael Varane pamoja na kiungo kutoka England Jadon Sancho.

Ada ya usajili wa Varane anayeitumikia Real Madrid inatajwa kufikia kiasi cha Pauni milioni 50, huku Sancho anaemilikiwa na Borussia Dortmund ya Ujerumani ada yake ni Pauni milioni 75.

Olympic Japan: Kocha wa timu ya Uganda akutwa na Corona
Akamatwa akichukua damu kwenye mwili wa marehemu